<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Ni siku kuu siku ile TZR56</title>
<lyrics>[V1]
 Ni siku kuu siku ile
 Ya kumkiri Mwokozi!
 Moyo umejaa tele,
 Kunyamaza hauwezi.

[V2]
 Siku kuu! Siku kuu!
 Ya kuoshwa dhambi zangu kuu!
 Hukesha na kuomba tu,
 Ananiongoza miguu.
 Siku kuu! siku kuu!
 Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

[V3]
 Tumekwisha kupatana
 Mimi wake, yeye wangu,
 Na sasa nitamwandama,
 Nikiri neno la Mungu.

[V4]
 Moyo tulia kwa Bwana
 Kiini cha raha yako,
 Huna njia mbili tena;
 Yesu ndiye njia yako.

[V5]
 Nadhiri yangu ya mbele
 Nitaiweka daima,
 Hata ije siku ile,
 Ya kuonana kwa salama</lyrics>
<hymn_number>56</hymn_number>
</song>